KOMPYUTA
JE KOMPYUTA YAKO INA HITILAFU / IMEHARIBIKA ?
Maranyingi watu wengi wanaonunua vifaa hivi vya teknolojia huwa na malengo mazuri sana, hususani ya kibiashara. Lakini kumekuwa na shida kubwa sana kwa watu wanaomiliki kompyuta na vifaa ambata kutokuwa na mpango mkakati wa kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara hali inayopelekea kupata hasara ya kufa kwa vifaa hivi na kupelekea hasara katika biashara zao pia.
Mtunzo makubwa ambayo yanatakiwa kufanyika mara kwa mara ili kuokoa kompyuta isiharibike ni pamoja na;
1. Kuhakikisha kompyuta inatumika mahali penye hali ya hewa nzuri na yakutosha
2. Kuhakikisha kompyuta yako inafutwa vumbi angalau mara tatu kwa mwaka kwa vifaa maalumu
3. Heat sink inabadilishwa angalau mara moja kwa mwaka
4. Antivirus inabadilishwa kwa wakati kulingana na mkataba wa manunuzi
5. kuhakikisha unahifadhi kumbukumbku zako katika kifaa mbadala ili kupunguza mzigo wa data
6. Kama ni Desktop isihamishwe hamishwe wala kuchomoa chomoa nyaya bila sababu za msingi
7. Hakikisha umeme unapozwa kabla ya kuingia katika kompyuta, tumia UPS au Stablelizer
8. Hakikisha kompyuta ina kuwa na Nywila ili wasiohusika wasiweze kuchezea
9. Hakikisha kila baada ya masaa 4 inazima ili kuipumzisha mashine hasa kwa wanaotumia mtandao
10.Hakikisha mahali ulipoweka kompyuta yako hapanya maji au unyevunyevu
11. Hakikisha Extension unayotumia kwa kompyuta haichomekwi vitu vingine kama vile pasi, heater nk
Kwa ujumla unatakiwa unaponunua kompyuta na vifaa vingine kwa ajili ya biashara au shughuli binafsi, basi unaweka mpango mkakati wa kuvitunza ili ufaidike navyo.
Ikiwa unajitahi huduma ya matengenezo au ushauri wa namna nzuri ya kuhifadhi vifaa vyako vya teknolojia tuwasiliane kwa anwani zetu hapo juu ili tuweze kukusaidia;
Kazi tunazofanya ni pamoja na;
-Kutengeneza kompyuta zilizoharibika ( computer Repair)
-Kutengeneza Printer zilizoharibika (printer repair)
-kutengeneza Thermoal Printer (thermal printer repair)
-Kufunga Netweki (Network -LAN- Installation)
-Kufunga Simu (phone Installation)
- Kufunga kamera za ulinzi ( Security Camera Installation)
-Kuboresha mifumo ya kompyuta (System Upgrade )
-Kubadilisha vifaa vilivyoharibika (Hardware and Software Installation)
-Mafunzo ya kompyuta (Technical Hardware and Software Training)
Huduma hizi unaweza kufanyiwa mahali popote ulipo hususani mikoa yote yaTANZANIA






Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali zingatia maadili unapotoa maoni