MUZIKI
JE UNAPENDA KUJIFUNZA KUTENGENEZA MUZIKI ?
Vijana wengi kwa sasa wanatamani kujifunza muziki, kutengeneza muziki na hata kusimamia shughuli za muziki. Jambo hili linaonekana ni rahisi sana hasa kwa sababu, moja kila mtu anaamini anajua kuimba, pili, muziki unafanywa na watu wengi ambao hawakusoma elimu za juu(waimbaji) , tatu, kila mtu ananafasi ya kufanya muziki. Lakini Je? Wanafanya muziki kwa usahihi?, Wanafanya muziki wa kibiashara?...... Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza kama unapenda kujifunza muziki.
Sekta hii ya muziki ina ina mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine inatoa fursa za ajira kwa watu mbalimbali, lakini ningependa kuzungumzia fursa tatu kubwa ambazo kwa sasa ni ajira rasmi ama za kuajiriwa au za kujiajiri….
1. Kuzalisha muziki (Producer)
2. Kuimba ( Artist)
3. Usimamizi wa muziki (Management)
1.KUZALISHA MUZIKI (PRODUCER)
Hili ni eneo mojawapo katika sekta ya muziki ambalo kwa sasa limekuwa ajira rasmi kwa watu mbalimbali hususani vijana. Je ni nani anafaa kuwa mzalishaji wa mziki (Producer) Jibu : Mtu yoyote mwenye akili timamu na umri wowote ule anaweza kuwa mzalishaji wa muziki (Producer)
Kwa ulimwengu wa Technolojia wa sasa uzalishajii wa muziki umerahisishwa sana hasa kwa kutumia kompyuta na vifaa vingine. Watu wengi wanafikiri ni lazima uwe umesoma kompyuta ndo uanze kuzalisha muziki! Hili si kweli uwe unajua ama hujui kutumia kompyuta bado unayo nafasi na unaweza kujifunza kuzalisha mzuki.
Kwa wale wanaojua kupiga vyombo vya mziki na wasiojua,wale wanao imba na hata ambao hawakuwa na mvuto na mziki bado wanaweza kujifunza program yoyote ya mziki na wakawa wazalishaji wazuri kwa muda mfupi.
Sasa tuangalie mambo muhimu ya kuzingatia (Vifaa) iliuweze kuwa mzalishaji wa muziki (producer) ni pamoja na ;
1. Kompyuta
2. Spika Maalumu (Monitor)
3. Kadi sauti ( sound card)
4. Spika za sikio (Headphones)
5. Kinasa sauti (condenser mic)
6. Stendi ya mic (mic stand)
7. Kinanda (Piano)
8. Programu ya muziki (DAW)
Jabo muhimu zaidi hapa ni kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinatumika katika chumba maalumu kinaitwa STUDIO ROOM.
Chumba hiki huwa kinajengwa kitaalamu ili kuhakikisha muziki unaozalishwa unakuwa na ubora wa viwango vya juu hasa linapokuja swala la kibiashara.
JE UNGEPENDA KUJIFUNZA NA UWE MZALISHAJI WA MUZIKI ?



Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhali zingatia maadili unapotoa maoni