VIDEO

JE UNAPENDA KUJIFUNZA VIDEO EDITING ?

Vijana wengi kwa sasa wanatamani kujifunza kuigiza, kutengeneza filamu na hata kusimamia shughuli za filamu. Jambo hili linaonekana ni rahisi sana hasa kwa sababu, moja kila mtu anaamini anajua kuigiza, pili, filamu inafanywa na watu wengi ambao hawakusoma elimu za juu(Waigizaji) , tatu, kila mtu ananafasi ya kufanya filamu. Lakini Je? Wanafanya filamu kwa usahihi?, Wanafanya filamu za kibiashara?...... Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza kama unapenda kujifunza kuhusu filamu.

Sekta hii ya filamu ina ina mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine inatoa fursa za ajira kwa watu mbalimbali, lakini ningependa kuzungumzia fursa tatu kubwa ambazo kwa sasa ni ajira rasmi ama za kuajiriwa au za kujiajiri….
1. Kuzalisha filamu          (director)
2. Kuchukua picha           ( Video shooting)
3. Usimamizi wa filamu   (Management)

1.KUZALISHA FILAMU  (DIRECTORS)

Hili ni eneo mojawapo katika sekta ya filamu ambalo kwa sasa limekuwa ajira rasmi kwa watu mbalimbali hususani vijana. Je ni nani anafaa kuwa mzalishaji wa filamu (Director) Jibu : Mtu yoyote mwenye akili timamu  na  umri wowote ule anaweza kuwa mzalishaji wa filamu(Director)

Kwa ulimwengu wa Technolojia  wa sasa uzalishajii wa filamu umerahisishwa sana  hasa kwa kutumia kompyuta,kamera za digitali na vifaa vingine. Watu wengi wanafikiri ni lazima uwe umesoma kompyuta au digitali katika picha za mnato(video) ndo uanze kuzalisha filamu! Hili si kweli uwe unajua ama hujui kutumia kompyuta bado unayo nafasi na unaweza kujifunza kuzalisha filamu.
Kwa wale wanaojua kutumia vyombo vya filamu na wasiojua,wale wanao cheza filamu na hata ambao hawakuwa na mvuto na filamu bado wanaweza kujifunza  program yoyote ya filamu na wakawa wazalishaji wazuri kwa muda mfupi.


Sasa tuangalie mambo muhimu ya kuzingatia (Vifaa) iliuweze kuwa mzalishaji wa filamu (Director) ni pamoja na ;
1. Kompyuta
2. Spika Maalumu (Monitor)
3. Kadi sauti  ( sound card)
4. Spika za sikio (Headphones)
5. Kinasa sauti (condenser mic)
6. Stendi ya mic (mic stand)
7. Kinanda           (Piano)
8. Programu ya muziki (DAW)
9.     kamera              (high quality camera)
10.   Vizuizi mionzi (sun reflectors)
Jabo muhimu zaidi hapa ni kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinatumika katika mazingira maalumu ili kuhakikisha unapata filamu zilizo bora na mwonekano wa kuvutia.

 Chumba cha kueditia filamu huwa kinajengwa kitaalamu ili kuhakikisha filamui unayozalishwa inakuwa na ubora wa kiwango cha juu hasa linapokuja swala la kibiashara.

JE UNGEPENDA KUJIFUNZA NA  UWE  MZALISHAJI WA FILAMU ?

JAZA FOMU KUJIUNGA                       RUDI MWANZO........

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE UNAPENDA KUJIFUNZA VIDEO EDITING ?

JE UNAPENDA KUMILIKI STUDIO YAKO?

JE UNAPENDA KUJIFUNZA KUTENGENEZA MUZIKI ?