STUDIO

JE UNAPENDA KUMILIKI STUDIO YAKO?

Studio ni mahali ambapo huwa panaandaliwa maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi mbalimbali kama vile stesheni za Redio, kuandaa muziki, filamu na hata kufanyia mahojiano ya vipindi mbalimbali vya televisheni.

Hapa nitazungumzia zaidi kuhusu Studio za kuzalisha Muziki (Music production Studio). Jambo kubwa ambalo ningependa ufahamu ni  kwamba utengenezaji wa muziki ni fani kubwa sana Afrika Mashariki  na Duniani kwa sasa. zipo kozi mbalimbali zinazofundisha maswala haya ya muziki katika vyuo mbalimbali duniani na mojawapo ya kozi hizo ni Sound Engineering.
Watu wengi wamejifunza maswala ya muziki kwa namna mbalimbali, ikiwemo kwenda shule au kujifunza kupitia watu wanaojua (formal and Informal music education).  Lakini pamoja na kuufahamu muziki, mazingira wanayofanyia shughuli wa uzalishaji wa muziki ni duni kiasi kwamba hata muziki unaozalishwa hauwi na kiwango cha kupelekwa katika masoko ya dunia. TATIZO NI NINI?
Kuna sababu mbalimbali zinazopelekea mazingira ya Studio nyingi kuwa chini ya kiwango ambazo yaweza kuwa;
-Kutokuwa na uelewa wa umuhimu wa kuboresha Studio
-kutafuta pesa za harakaharaka
-kutokuwa tayari kufanya biashara ya ushindani
-kutokuwa na malengo makubwa
-Kujifurahisha kumiliki studio
-kukosa pesa za vifaa
-kutokuwa na eneo la uhakika n.k
Pamoja na sababu mbalimbali tajwa hapo juu, bado kuna umuhimu wa kuwa na studio inayokidhi mahitaji ya soko la ushindani kibiashara. Studio inaweza ikawa kubwa au ndogo kulingana na uwezo wako ila kinachoangaliwa zaidi, ni kuwa studio bora ambayo inaweza kuzalisha Muziki mzuri ambao utaleta faida kwa mmiliki au mtengenezaji wa muziki (Producer)

Kuna mahitaji mbalimbali ili uweze kuandaa studio iliyobora na itakayokuwezesha kufanya kazi nzuri;
-Mbao
-Sponji
-roofsheet
-Kapeti la sponji
-Voice Absobers
-Acoustic pannel
-Booth Materials
-Gundi
-Vioo
- vifaa vya mawasiliano
Hoyo ni baathi ya mahitaji kwa ajili ya ujenzi wa Studio, ila cha kizingatia hapa ni kwamba uwingi wa mahitaji huwa unategemeana na ukubwa wa studio.

JE UNATAMANI KUWA NA STUDIO YENYE KIWANGO CHA KIMATAIFA ? 

JAZA FOMU KUJIUNGA                       RUDI MWANZO......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE UNAPENDA KUJIFUNZA VIDEO EDITING ?

JE UNAPENDA KUMILIKI STUDIO YAKO?

JE UNAPENDA KUJIFUNZA KUTENGENEZA MUZIKI ?