PICHA


JE UNAPENDA KUJIFUNZA KUPIGA / KUEDITI PICHA ?

Upigaji wa picha za mgando ni moja kati ya fani muhimu sana nyakati za sasa, wakati ambapo Biashara nyingi kwa kiasi kikubwa zinfanywa hasa kwa kutumia mitandao. Awali upigaji wa picha za mgando ulikuwa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu kwa shughuli na matukio ya kijamii, kisiasa,kiutamaduni na kiutafiti hasa wa kisayansi.

Lakini kwa wakati huu picha za mgando zimekuwa ni bidhaa yenye thamani kubwa sana kutokana na mapinduzi ya biashara mtandao, ambapo kwa kiasi kikubwa picha za mgando zinztumika katika kutangaza na kutambulisha bidhaa mbalimbali katika soko kubwa la biashara mtandao ikiwemo Utalii.
Awali wakati picha za mgando zilikuwa zinapigwa kwa ajili ya matukio ya kijamii zaidi na kisayansi hakukuwa na ubunifu mkubwa kwa wapiga picha  kwa sababu picha hizi zilikuwa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu tu. 

Lakini baada ya kukua kwa technolojia na matumizi ya kompyuta kuongezeka miongoni wa wanajamii mbalimbali Duniani, wafanyabiashara wakatumia hii fursa ya kukua kwa matumizi ya teknolojia na kutanuka kwa uwanda wa mawasiliano kupitia mitandao katika kuuza bidhaa zao. Jambo hili likapelekea kutafutwa kwa namna nzuri ya kuwasilisha bidhaa kimtandao (branding), ili bidhaa zinazowasilishwa kwa watu ziwe na mvuto,hivyo kurahisisha  uuzaji wa bidhaa hizo.
Hapo ndipo ubunifu mkubwa wa upigaji picha ukaibuka kwa kasi na soko la picha za namna hii kuongezeka kwa kasi pia. hali hii imesababisha sasa hata picha za shughuli za kijamii, kiutamaduni,kisiasa na kisayansi kufuata mkondo huo katika namna ya kupata kumbukumbu iliyobora, jambao ambalo limepelekea upigaji picha kuwa SANAA kubwa Duniani.

Picha hizi zinapigwa kwenye Sherehe mbalimbali kama Harusi, Maazimisho mbalimbali, Mahafari mabalimbali, shughuli za misiba, kupiga (graphic brand) bidhaa mbalimbali na mwishowe kwa upande wa biashara bidhaa huwekwa katika mitandao mbalimbali kwa ajili ya kuuzwa ama kutangazwa.
Ili ujifunze kupiga picha na kuediti (PHOTOGRAPHER AND GRAPHICS DESIGNING) unatakiwa kuwa na mahitaji yafuatayo
1. Kamera (Digital camera)
2. Kompyuta (computer)
3. Stendi ya Kamera (Camera stand)
4. kutuna kumbukumbu (External storage)
5. programu ( Graphic Software)
6. Taa za mwanga (lights)
7. Printer  za Picha (proffessional printer)
Shughuli hii mtu yoyote anaweza kujifunza na kuanza kufanya kazi katika kipindi kifupi hususani katika kutangaza bidhaa za kibiashara katika mitandao mbalimbali na kuweza kujiajiri ili kupata kipato cha kutosha.


JE UNGEPENDA KUJIFUNZA NAMNA NZURI YA KUPIGA PICHA NA KUEDITI ?

JAZA FOMU KUJIUNGA                      RUDI MWANZO.......

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE UNAPENDA KUJIFUNZA VIDEO EDITING ?

JE UNAPENDA KUMILIKI STUDIO YAKO?

JE UNAPENDA KUJIFUNZA KUTENGENEZA MUZIKI ?